Polisi Marekani wamemfungulia mashtaka kiongozi wa genge la
uhalifu, kwa mauaji ya rapa Tupac Shakur mwaka 1996, yaliyoacha maswali mengi
kwa umma kwa muda mrefu.
Msanii huyo mashuhuri wa muziki wa hip-hop aliyezaliwa Jijini
New York Marekani, alipigwa risasi nne na kufa akiwa kwenye gari barabarani
huko Las Vegas.
Ijumaa, Mahakama ya Juu ya Nevada, imemfungulia kesi Duane
"Keffe D" Davis, 60, akikabiliwa na shtaka la mauaji hatari ya
kutumia silaha.
Polisi wamesema Keffe D, alipanga mauaji hayo ya Tupac baada
ya binamu yake kugombana na Tupac Shakur kwenye Casino.
Duane "Keffe D" Davis alikamatwa nyumbani kwake Las
Vegas mapema jana na atafikishwa mahakamani katika siku za hivi karibuni.
Picha iliyotolewa na Polisi Marekani ikimuonyesha kiongozi wa genge la uhalifu Duane "Keffe D" Davis, anayeshtakiwa kwa mauaji ya rapa Tupac Shakur
0 Maoni