Mjukuu wa kike wa Nelson Mandela afariki kwa saratani

 

Zoleka Mandela, mjukuu wa rais wa kwanza aliyechaguliwa Kidemokrasia Afrika Kusini, Nelson Mandela, amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 43.

Zoleka amefariki dunia jumatatu jioni akiwa amezungukwa na marafiki pamoja na familia yake, Msemaji wa familia ya Mandela ameeleza.

Katika miaka ya hivi karibuni, Zoleka alifahamika kwa kuelezea vyema umma matibabu ya saratani anayopatiwa. Pia aliweka wazi historia yake ya kuwahi kuwa teja wa dawa za kulevya.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni