India yakanusha kumuua kiongozi wa Sikh wa Canada

 

Nchi ya India imekanusha vikali tuhuma za Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, za kuhusika katika kifo cha kiongozi wa dhehebu la Sikh wa Canada.

Jumatatu, Trudeau aliituhumu India kwa mauaji ya Hardeep Singh Nijjar, ambaye alipigwa risasi na kufa nje ya hekalu la Sikh, Juni 18 huko Canada.

Waziri Mkuu Trudeau amesema vyombo vya kiitelijensia vilikuwa vinaangalia tuhuma za kifo cha kiongozi huyo kuhusishwa na taifa la India.

Siku ya Jumanne, India ilimfukuza balozi wa Canada nchini India, na kuchochea mgogoro wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo.

Hatua hiyo ya India inafuatia uamuzi wa Canada kumtimua balozi wa India Pavan Kumar Rai kuhusiana na tukio hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni