Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa azindua mradi wa maji wa kitama Wilayani Tandahimba Mkoani
Mtwara. Mradi huo umegharimu thamani ya shilingi Milioni 798.7.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb)
katika hafla hiyo amesema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tank
la lita laki 100, ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 20.1, ujenzi wa vioski 10
vya kuchotea maji
Pia Mhe. Mahundi ameeleza kuwa Serikali imeanza utekelezaji
wa mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika miji 28 ambapo kwa Wilaya ya
Tandahimba mkandarasi ameshaanza utekelezaji wa mradi wa Makonde kwa gharama ya
shilingi Bilioni 84 ambapo mpaka sasa Mkandarasi amepewa shilingi Bilioni 12
kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo.
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu amepongeza Wizara
ya Maji kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji Nchini na
kusisitiza kuwa wananchi waendelea kulinda miundombinu ya maji pamoja na
kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ili miradi hii inayotekelezwa kwa Awamu ya
Sita iwe endelevu.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe. Ahmed Katani Katani
ameishukru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mingi ndani ya jimbo lake ukiwepo
mradi wa miji 28 wa Makonde ambapo kukamilika kwako kutaboresha huduma ya maji
katika Wilaya ya Tandahimba.
0 Maoni