Simba waliozua taharuki maeneo mbalimbali ya vijiji vya
mikoa ya Njombe na Iringa wameuawa leo tarehe 7 Agosti 2023 kitongoji cha Lole
Kijiji cha Makungu Wilaya vya Mufindi kwa ushirikiano wa askari wa Jeshi la
Uhifadhi wa wanyama pori toka Kipengere
Mkuu wa Hifadhi ya Wanyama Pori Kipengere Mkoani Njombe Bw. Donasiani
Makoye amesema simba hao walitoweka hifadhini mnamo tarehe 21 Julai 2023.
Na wao kama Jeshi la Uhifadhi waliendelea kuwafuatilia simba
hao na leo hii tarehe 7 Agosti 2023 wamefanikiwa kuwauwa
Mhifadhi huyo amekiri kuwa Simba hao wamesababisha madhara
makubwa kwa kushambulia na kuuwa ng'ombe 14 na nguruwe 5 hadi kuuawa kwao hii
leo.
Aidha, Mhifadhi huyo amesema wao Jeshi la Uhifadhi
wanaendelea kuchukua hatua zaidi ili kuwadhibiti simba hao ikiwa pamoja na kuwafungia
mfumo wa mawasiliano wa utambuzi
Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Makungu wamesema kwa muda
mrefu wameshindwa kuendelea na majukumu yao kwa kuhofia simba hao wakiendelea
kuongea na Mufindi Fm Radio wananchi hao wamesema wanawashukuru askari hao wa
Hifadhi ya Kipengere kwa kuwauwa simba hao na kutoa rai kwa serikali na mamlaka
husika kuja na namna sahihi ya kuwadhibiti simba hao wasitoke kwenye hifadhini.
Na. Anton Kuyava- Mufindi Fm Radio
0 Maoni