Messi aendeleza moto wa kufumania nyavu akiwa na Miami

 

Lionel Messi amefuta hofu ya kuumia na kufunga goli lake la tisa katika michezo sita akiwa na Inter Miami, wakiifunga Philadelphia Union na kutinga fainali ya kombe la ligi.

Raia huyo wa Argentina mshindi wa kombe la dunia aliifungia Miami goli la pili katika ushindi wa magoli 4-1, siku moja tu baada ya kuumia kwenye enka mazoezini.

Josef Martinez, Jordi Alba na David Ruiz nao waliifungia magoli Miami, huku naye Alejandro Bedoya akiwafungia wenyeji goli pekee.

Chapisha Maoni

0 Maoni