Kiungo Mbrazili Fabinho amekamilisha uhamisho wa kuhamia
klabu ya Saudi Arabia ya Al-Ittihad kutoka Liverpool.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, hakuwepo kwenye kambi
ya Liverpool waliyokaa Ujerumani, baada ya timu hiyo ya Saudi kutoa ofa ya paundi
milioni 40.
Fabinho pia aliachwa na Liverpool katika safari yao ya
Singapore kwa lengo la kumuwezesha kukamilisha mpango wake wa kuhamia Al-Ittihad.
0 Maoni