Mtuhumiwa mauaji mjamzito Vingunguti adakwa Polisi wasimulia kisa kizima


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Julai 31, 2023 limewakamata watuhumiwa saba akiwemo Amani Kipolo mkazi wa Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kusababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane (8).

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema Watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati wakitoka kuzimka mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino.

Aidha, awali marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023.


Katika tukio jingine Jeshi hilo limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya (18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi wakuu wa Serikali Tanzania kwa kutumia mitandao ya kijamii.

 

Mtuhumiwa huyo  alikamatwa Julai 29, 2023, na wenzake wamekuwa wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok. 


Kamanda Muliro amesdma Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani huku akitoa onyo kali kwa mtu/ watu wanao toa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria.

Chapisha Maoni

0 Maoni