Malengo ya SMZ kwa wananchi ni huduma bora za afya Zanzibar- Dk. Mwinyi

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo ya Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora za afya.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 wakati akifungua kituo cha afya Bumbwini Makoba, Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza katika hatua za awali zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora kufikia malengo ya kuimarisha miundombinu kwa kujenga hospitali za Wilaya kila Wilaya, hospitali za Mkoa kila Mkoa na hospitali ya Binguni itakayokuwa kubwa zaidi na kutoa huduma za uchunguzi Zanzibar.

Pia hatua nyengine Serikali imeamua kushirikiana na sekta binafsi zitoe huduma katika hospitali za serikali zinazohusisha uchunguzi wa maradhi mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni