Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewataka wakulima wa miwa kuendelea kulima miwa kwa wingi kwani soko la miwa limekuwa kubwa kutokana na ongezeko la viwanda vya sukari nchini.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo jana. alipotembelea kiwanda cha
Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kujionea maendeleo
ya uzalishaji wa Sukari Pamoja na upanuzi wa Kiwanda hicho.
Dkt. Kijaji amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita
chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Miwa inayolimwa na wakulima
wadogo wa maeneo ya jirani na kiwanda iweze kununuliwa yote na kuchakatwa kwani
soko la miwa lipo na linaendelea kukua kila siku kutoka Tani la nane na
kuongezeka kwa Tani laki tisa nyingine ndani ya Kiwanda cha Kilombero.
Aidha ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na
Biashara inaendelea kufanya kazi nzuri ya kusimamia Mpango wa uboreshaji wa
Mazingira bora ya Uwekezaji na Ufanyaji Biashara Nchini unaofahamika kama
MKUMBI hali inayofanya kuwepo kwa wawekezaji wengi wa viwanda ndani ya
Tanzania.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amempongeza
Dkt.Kijaji kwa ziara yake hiyo katika Kiwanda hicho Pamoja na Kusimamia vyema
masuala ya viwanda na biashara hali iliyopelekea uongozi kupanua kiwanda hicho kwa
kuwekeza tena zaidi ya fedha za Kitanzania Bilioni 600 ili kuongeza uzalishaji
wa sukari chini.
0 Maoni