Zoezi la wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari hifadhini
Ngorongoro limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa kundi jipya lenye mtazamo
tofauti linalotaka kuruhusiwa kuhamia wanakotaka wenyewe kwa sharti tu la
Serikali kuwalipa fidia zao na kuwahamisha
Baadhi ya wakazi wa vijiji kadhaa wenye mtazamo huo wanasema
wao wapo kila sehemu Tanzania nakwamba ni vyema Serikali ikatoa uhuru huo wa
wao kwenda wanakotaka
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Erkepusi Mbokieni Sapuo
anasema yeye na familia yake wamechagua kwenda uelekeo wa Engaruka ambapo
tayari kuna ndugu zao wengine wanaishi huko muda mrefu
"Tunaomba turuhusiwe kuhamia popote nje ya Ngorongoro
bila ya kwenda Msomera."
"Tunaiomba Serikali itupe fidia sisi tunataka kuhama
lakini sio lazima twende kulikopangwa na Serikali."
"Pawe na uhuru wa mtu kuchagua kama anataka kwenda
Msomera sawa, kama anataka kwenda Kitwai sawa na kama hataki kwenda kokote kati
ya huko sawa".
"Mimi nataka niende maeneo ya Engaruka, Serikali
inifidie niende na ndugu zangu." Amesema Sepuo
Itakumbukwa kwamba tayari kaya zaidi ya 500 zimehama kwa
hiyari kuelekea Msomera, Handeni mkoani Tanga na Serikali imetangaza kuanza kwa
mchakato wa ujenzi wa nyumba nyingine 5000 katika maeneo ya Msomera, kilindi na
Kitwai Kwa ajili ya kuwahakikishia wakazi wa Ngorongoro wanaoendelea
kujiandikisha Kwa hiyari.
Kuibuka kwa kundi hili linalotaka kuhamia mahala wanapotaka
wenyewe ni mwendelezo wa kueleweka kwa zoezi hilo muhimu kwa UHIFADHI na Ustawi
wa maisha yao.
Na. Mwandishi Wetu- Ngorongoro
0 Maoni