Ajabu kontena lililokuwa na wine lakutwa na chupa tu bandarini

 

Kweli dunia haishi maajamu. Huko Kenya kontena la futi 40 lililoagizwa kutoka nje likiwa na pombe limekutwa likiwa na chupa tupu, wakati wa zoezi la kuhakiki bidhaa iliyokuwamo lililofanywa na Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA).

Kontena hilo ni mingoni mwa makontena 104 yaliyokuwa na bidhaa zilizoisha muda wake wa kutumika likiwa limeorodhoshwe ili bidhaa hiyo ya mvinyo (wine) iteketezwe katika Bandari ya Mombasa baada muagizaji wake kushindwa kulipa ushuru kwa wakati.

Bidhaa zingine zilizokuwamo kwenye makontena hayo 104 ni za vyakula kama vile mchele, ngano, maziwa pamoja na juisi zilikuwa zimehifadhiwa tangu kuanzia mwaka 2008 hadi 2021, zikingoja kuteketezwa.

Katika notisi iliyochapishwa kuhusiana na kontena hilo, mamalaka za nchini Kenya zimesema kwamba kontena hilo lililokuwa na shehena ya mvinyo (wine) liliingizwa nchini Kenya mnamo Julai 29, mwaka 2009.

Kumekuwapo na tuhuma kuhusu maafisa wa mamlaka ya bandari Kenya, kushirikiana na waagizaji wa bidhaa kutorosha bidhaa zinazoshikiliwa kwa ajili ya kushindwa kulipiwa ushuru na ambazo zimeisha muda wake wa kutumika.

Chapisha Maoni

0 Maoni