Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu afanyiwa upasuaji wa moyo

 

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, amefanyiwa upasuaji wa dharura na kuwekewa kifaa cha kurekebisha mapigo ya moyo (pacemaker) baada ya kupelekwa hospitali usiku wa Jumamosi.

Madaktari wa hospitali ya Shena Medical Centre wamesema upasuaji huo umefanyika vizuri, na Netanyahu hayupo katika hali ya kuhatarisha maisha yake.

Kuugua na kulazwa hospitali Bw. Netanyahu, kumekuja wakati ambao bunge la nchi hiyo linaelekea kupiga kura muhimu ya mabadiliko ya mfumo wa Mahakama.

Maandamano yanayopinga mabadiliko hayo yamesambaa Israeli, huku wafanyakazi wengi wakiapa kugoma iwapo muswada huo utapitishwa na bunge.

Chapisha Maoni

0 Maoni