KOMBE LA DUNIA WANAWAKE: Uholanzi yaichapa Ureno

 


Goli la kwanza la Stefanie van der Gragt katika kipindi cha kwanza, limeipatia ushindi wa goli 1-0 timu ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Ureno kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake huko Dunedin.

Mpira wa kichwa cha nguvu uliopigwa na Van der Gragt, ulidhaniwa kuwa umetoka nje na muamuzi Kateryna Monzul kabla ya refa msaidizi kumsihi aangalie marudio kwenye video na kubadili uamuzi wake.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno walishindwa kuisumbua ngome ya Uholanzi, ambapo walipata shuti moja pekee lililolenga goli mnamo dakika ya 82 ya mchezo huo.

Kwa ushindi huo umeifanya Uholanzi kushika nafasi ya pili kwenye kundi E, ikiwa nyuma ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya taifa ya wanawake Marekani, kwa tofauti ya magoli ya kufunga.

Chapisha Maoni

0 Maoni