Luis Miqissone sasa rasmi ndani ya klabu ya Simba

 


Mchezaji Luis Miqissone amerejea tena klabu ya Simba, ikiwa ni baada ya kutumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa kabla ya kuuza kwa miamba ya soka Afrika Al Ahly ya Msiri miaka miwili iliyopita.

Hatua hii inamaliza uvumi wa muda mrefu kuwa mchezaji huyo atarejea Simba, na leo hii Simba wamemtambulisha rasmi baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo huyo mshambuliaji raia wa Msumbiji kutoka Al Ahly kwa mkataba wa miaka miwili.

Msemaji wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Miquissone anarejea Simba tena baada ya kuitumikia Simba kwa mafanikio makubwa, kabla ya kuuzwa kwa miamba ya soka Afrika Al Ahly.

Mchezaji Luis Miqissone amesajiliwa na Simba SC akiwa ni mchezaji huru, baada ya kuvunja mkataba na timu ya Al Ahly ya Misri.


Chapisha Maoni

0 Maoni