Wanajeshi wa nchi ya Afrika ya Magharibi ya Niger
wametangaza kufanya mapinduzi kupitia televisheni ya taifa.
Wanajeshi hao wamesema wameifuta Katiba, na kusitisha
shughuli zote za taasisi pamoja na kufunga mipaka yote ya nchi hiyo.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum, anashikiliwa na vikosi maalum
vya ulinzi wa rais tangu mapema siku ya Jumatano.
Marekani imemuahidi kumpatia ushirikiano usio na shaka, kwa
njia ya simu iliyopigwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres naye amesema
ameongea na rais Bazoum na kumuhakikishia kuwa Un inamuunga mkono.
Rais Bazoum wa Niger ni mdau muhimu wa mataifa ya magharibi
katika mapambano dhidi ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu Afrika ya
Magharibi.
0 Maoni