Mwanamke kuuawa kwa kosa la dawa za kulevya Singapore

 

Nchi ya Singapore, inapanga kutekeleza adhabu ya kifo kwa mwanamke kwa mara ya kwanza baada ya karibu miaka 20 kupita, wakili wa haki za binadamu amesema.

Mwanamke huyo raia wa Singapore Saridewi Djamani, 45, alitiwa hatiani kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 30 mnamo mwaka 2018.

Mwanamke huyo atakuwa mtu wa pili kuuawa kwa kosa la dawa za kulevya katika siku tatu baada ya Mohd Aziz bin Hussain kuuawa, na mtu wa 15 kuuawa tangu Machi 2022.

Singapore ni moja ya mataifa yenye sheria kali za kukabiliana na dawa za kulevya duniani, ambayo wanasema ni muhimu katika kuilinda jamii.

Chapisha Maoni

0 Maoni