Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), inatarajia kuanza
kutoa huduma ya kuzibua mishipa ya uume ikiwa ni hatua ya kukabiliana na
upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wenye tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa JKCI Dk. Peter Kisenge, amesema huduma hiyo inatarajiwa kuanza
mwezi Oktoba mwaka huu.
Dk. Kisenge amesema tatizo hilo ni kubwa japo hakuna utafiti
walioufanya, lakini wapo wanaume wenye tatizo hilo wanaofika kwenye taasisi ya JKCI.
“Tutakwenda kuanzisha huduma mpya ambapo tutashirikiana na
wenzetu wa India, kwani tatizo la nguvu za kiume linazidi kuongezeka kwa
mishipa ya uume kuziba,” amesema Dk. Kisenge.
Dk. Kisenge amesema “tatizo lipo na pengine hilo ni siri ya
wagonjwa hatuwezi kuweka wazi ila huduma itaanza mwaka huu”.
0 Maoni