Wakurugenzi na viongozi wengine waondolewe mamlaka ya kipolisi

 


Tume imependekeza mamlaka ya kipolisi ya kukamata na kuweka mtuhumiwa kizuizini waliyonayo Wakurugenzi wa Halmashauri na Maofisa Watendaji wa Kata yaondolewe na jukumu hilo liachwe kwa Jeshi la Polisi.

Mapendekezo hayo na mengineyo yametolewa na Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini, wakati ikiwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa Serikali.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Ikulu, Dar es Salaam na Mwenyekiti Tume ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande.

Jaji Mkuu Mstaafu Chande amesema tume imebaini kuwa mamlaka ya kukamata imetolewa kwa taasisi nyingi na kwa watu wengi ambao wamevishwa mamlaka ya kipolisi.

Chapisha Maoni

0 Maoni