Mvua kubwa zaua watu 22 Korea Kusini

 


Watu wapatao 22 wamekufa, kufuatia mafuriko makubwa Korea Kusini, wakati mvua kubwa zikiendelea kunyesha katika mikoa ya kati.

Katika siku ya tatu ya mvua kubwa, kumetokea maporomoko ya ardhi, na kusababisha bwawa kubwa katika mkoa wa Chungcheong kufurika maji.

Mvua hizo kubwa zimepelekea barabara kufunikwa na maji, magari kusombwa na maji, na kutatiza usafiri wa reli.

Watu wengine 14, wameripotiwa kutoweka na maelfu wamelazimika kuhama makazi yao, maofisa wa nchi hiyo wamesema.

Chapisha Maoni

0 Maoni