Joto kali lawatesa Wamarekani milioni 113, tahadhari yatolewa

 

Hali ya joto kali Marekani, imetabiriwa kuongezeka mwishoni mwa juma hili, huku tahadhari ikitolewa eneo la kusini magharibi mwa taifa hilo.

Hadi kufikia Ijumaa, joto hilo liliwaathiri Wamarekani milioni 113, huko Florida, Texas, California, hadi katika jimbo la kaskazini-magharibi la Washington.

Matumizi ya viyoyozi katika jimbo la Texas, yaliongezeka na kufikia kiwango cha juu katika jimbo hilo, na kuweka rekodi ya matumizi ya umeme.

Watu wapatao milioni 27 nchini Marekani wametabiriwa watalazimika kukabiliana na hali ya joto inayofikia nyuzi joto 43, katika siku zijazo.

Chapisha Maoni

0 Maoni