Wabunge wanaoshiriki mkutano wa SADC kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro

 

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ni miongoni mwa taasisi  zinazoshiriki maonesho ya utalii yanayoendelea katika Hotel ya Gran Melia jijini Arusha ambapo *Mkutano wa 53 wa Jukwaa la Mabunge la Nchi za SADC (53 SADC Parliamentary Forum) unafanyika kuanzia tarehe 2-8 Julai, 2023


Sambamba na mkutano huo, Wizara ya Maliasili na utalii imeandaa banda la maonesho ya vivutio vya utalii kwa kushirikisha taasisi zilizochini ya Wizara hiyo kwa lengo la kuelezea shughuli za Uhifadhi, fursa za uwekezaji na kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko maeneo mbalimbali nchini.


Mkutano huo unahusisha wajumbe zaidi ya sabini kutoka nchi 15 za SADC ambao utafuatiwa na ziara katika maeneo vivutio vya Utalii ambapo idadi kubwa ya wageni hao wamejiandikisha kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro siku ya Jumamosi tarehe 8 Julai, 2023.

Chapisha Maoni

0 Maoni