Tanzania Yashiriki Mkutano Shirika la Utalii UN Kanda ya Afrika

Ujumbe wa Tanzania jana umeanza kushiriki Mkutano wa 66 wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika (UNWTO-CAF) unaofanyika hapa nchini Mauritius.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambapo Tanzania pia inawania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji Ngazi ya Dunia pamoja na Kamati nyingine za kimkakati kwa Shirika hilo, umeongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Mary Msanja na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi.

Mkutano huo, pamoja na uchaguzi wa kwenda vyombo mbalimbali vya kikanda na dunia, pia utajadili hali ya Utalii Barani Afrika baada ya Uviko-19 na kujadili miradi ambayo Bara la Afrika itaipendekeza katika ngazi ya dunia na kujadiliwa katika Mkutano Mkuu wa UNWTO Oktoba mwaka huu.

Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano kama huo wa UNWTO kwa ngazi ya Afrika mwaka jana uliofanyika jijini Arusha.

Na Mwandishi Wetu, Mauritius

Chapisha Maoni

0 Maoni