KOMBE LA DUNIA WANAWAKE: Hispania yaipiga 5G Zambia

 

Jenni Hermoso na Alba Redondo wamefunga magoli mawili wakati Hispania ikiichakaza Zambia magoli 5-0 katika michuano Fifa ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Kwa ushindi huo Hispania imeionyesha dunia kuwa ni mingoni mwa timu inayoweza kutwaa kombe hilo, baada ya kutinga hatua ya 16 bora.

Wiki iliyopita Hispania ilianza michuano hiyo katika kundi C, kwa kupata ushindi rahisi wa magoli 3-0 dhidi ya Costa Rica.

Katika mchezo wa awali hii leo Japan iliichapa Costa Rica magoli 2-0, na kutinga hatua ya 16 bora ambapo timu hizo sasa zitakutana jumatatu kuwania kuongoza kundi C.

Chapisha Maoni

0 Maoni