Messi aanza kwa kufunga magoli mawili akiwa na Inter Miami

 

Lionel Messi atikisa nyavu mara mbili na kusaidia goli moja katika mchezo wake wa mwanzo akiwa na Inter Miami katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Atlanta United.

Nyota huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 36, alifunga magoli hayo mawili ndani ya dakika 22 za mwanzo na kumtengea goli Robert Taylor katika kipindi cha pili.

Baada ya kufunga goli lake la pili, Messi alishangilia kwa kumnyooshea kidole mmiliki wa Inter Miami mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza David Beckham.

Chapisha Maoni

0 Maoni