Moto wa nyika waua watu 40 Algeria, Italia na Ugiriki

 

Zaidi ya watu 40 wamekufa huko Algeria, Italia na Ugiriki wakati moto wa nyika wa Mediterranean ukielekea kuteketeza vijiji na hoteli za mapumziko, huku maelfu wakihamishwa.

Ugiriki inajiandaa kufanya zoezi la kuwaondoa watu zaidi kwa kutumia ndege kutoka Rhodes, wakati moto huo wa nyika ukishika kasi kueleka visiwa Corfu na Evia.

Joto lililopo kwa sasa linaonekana pia kutokushuka chini na badala yake linatarajiwa kupanda hadi kufikia nyuzi joto 44, katika maeneo ya Ugiriki.

Moto huo wa nyika pia umewalazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao kwenye miji ya Sicily na Puglia.

Upepo mkali pamoja na mimea mikavu imechangia kuwapa wakati mgumu zimamoto kuuzima moto huo na kukata maeneo ili moto usisambae.

Chapisha Maoni

0 Maoni