TANAPA, TAWA NA TAWIRI, zashirikiana kurudisha tembo hifadhini

 


Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo ni TANAPA, TAWIRI na TAWA leo tarehe 25.07.2023 wamefanya zoezi la kufukuza tembo kwenye maeneo ya wananchi ya Sarakwa na Tamau na kuwarudisha hifadhini.

Aidha, taasisi hizo pia zimefanya zoezi la kuwafunga tembo visukuma mawimbi “radio collar” likiwa na lengo la kufuatilia mienendo ya wanyama hao na kurahisha zaidi ufuatiliaji uwandani kwa askari wetu.

Chapisha Maoni

0 Maoni