Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, ameruhusu madaktari wa
hospitali za umma kufanya kliniki binafsi baada ya muda wa kazi kumalizika katika
hospitali za Serekali nchini.
Mhe. Ummy ametangaza uamuzi huo mkoani Simiyu wakati
akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa ya Simiyu katika ziara yake
aliyoifanya mkoani humo.
“Tusiweke urasimu daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu
afanyekazi zake za private (binafsi), wagonjwa wake wa private waje hapa
atawaona mtakubaliana percentage (asilimia ya malipo),” alisema Waziri Ummy na
kuongeza, “Hospitali ya Ocean Road nilifanya hivyo na MOI wewe mwenyewe unajua
vizuri, madaktari wa Dar es Salaam wanahangaika kweli kijiwe hiki kijiwe kile,
vijiwe hadi 120, daktari na muuguzi wanachoka sana”.
Mh. Ummy ameeleza kwamba kuna mgonjwa ambaye anataka aje kumuona
daktari wakati hamna fujo, akute chumba kizuri kinamakochi, kuna maji, kuna
chai, kuna kahawa, kuna soda na daktari atamuita muuguzi na kuchukua vipimo
vyote hapo hapo.
0 Maoni