Riyad Mahrez atimkia Al-Ahli ya Saudi Arabia

Mwanasoka Riyad Mahrez amekamilisha uhamisho kutoka Manchester City kwenda Ligi ya Saudi Pro katika timu ya Al-Ahli, kwa kitita cha paundi milioni 30

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anamuda wa miaka miwili uliobakia kwenye mkataba wake, anaingia kwenye orodha ya nyota wakubwa waliojiunga na ligi hiyo ya SPL.

Manchester City ililipa paundi milioni 60, kumnunua winga huyo raia wa Algeria 2018, na aliifungia magoli 15 katika michezo 47, City ikitwaa makombe matatu katika msimu uliomalizika.

Chapisha Maoni

0 Maoni