Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limevitaka vyombo vya
habari nchini kutopiga wimbo wa "Amkeni" uliotolewa hivi karibuni na
msanii wa BongoFleva, Emmanuel Elibariki Kingu, maarufu kama Ney Wa Mitego.
Kwa mujibu wa taarifa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), imepokea barua ya Kaimu Katibu Mkuu wa BASATA, John Daffa kwenda TCRA,
inayoagiza wimbo huo kutokupigwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo
vya habari nchini.
Kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana mwelekeo wa
kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo
hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla.
Barua hiyo ya Baraza la Sanaa Tanzania, pia imeongeza kuwa
wimbo huo wa "Amkeni" ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.
0 Maoni