Raila Odinga anaumwa asumbuliwa na mafua makali

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga anaumwa na kwa sasa ameagizwa na daktari wake kupata mapumziko.

Raila hajaonekana tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha pamoja na sheria mpya ya fedha ya 2023.

Akiongea kwa simu na gazeti la Nation Raila amesema ameanza kupata nafuu, na muda sio mrefu atarejea kwenye majukumu yake, baada ya kupona mafua makali.

Kuliibuka wasiwasi kuhusu alipo Raila Odinga jumatano, baada ya kushindwa kuonekana katika maandamano ya kulalamikia hali ngumu ya maisha.

Chapisha Maoni

0 Maoni