Ndege ndogo ya Jeshi la Wananchi Tanzania yaanguka Ziwa Victoria


Ndege ndogo ya jeshi iliyokuwa na marubani wawili yenye namba JW 9127 imeanguka Ziwa Victoria karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera wakati marubani hao wakiwa kwenye mazoezi ya kawaida.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa 3:30 asubuhi, wakati wanajeshi hao wakiwa kwenye mazoezi na ndipo ndege yao ilipoanguka kwenye Ziwa Victoria karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba.

Kamanda Chatanda amewataja marubani hao waliohusika kwenye ajali hiyo kuwa ni Leonard Nkundwa (45) na Alex Venance (30) ambao wamelazwa hospitali ya mkoa Bukoba wakipatiwa matibau chini ya uangalizi wa madaktari.

Mnamo Novemba 6, 2022 majira ya asubuhi ndege ya Shirika la Ndege la Precision, ilipata ajali Bukoba wakati ikijaribu kutua kwenye uwanja huo na kuanguka kwenye Ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19.

Wanajeshi wakiangalia ndege yao namba JW 9127 iliyoanguka leo kwenye Ziwa Victoria ikiopolewa kutoka majini.


Chapisha Maoni

0 Maoni