Prof. Muhongo aepusha malumbano aamua kujenga ukuta wa Makaburi Musoma

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameamua kujitosa mwenyewe kuendelea kujenga uzio wa makaburi yaliyopo eneo la Kanisa la Mennonite la Kitaji, Musoma Mjini yalikuwa hayana uzio.

Utuzwaji wa makaburi hayo ulikuwa ni mgumu kutokana na kukosekana kwa uzio, ndipo Prof. Muhongo alipotoa wazo la kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa makaburi hayo lakini michango ikawa midogo mno.

Hata hivyo kwenye wengi hapakosi changamoto, michango ya ujenzi ya uzio wa Makaburi hayo ilianza kusuasua na kama hiyo haitoshi kisha yakaibuka malumbano jambo ambalo lilimuhuzunisha Prof. Muhongo.

Kufuatia mvutano huo Prof. Muhongo aliamua michango isitishwe ili kuepusha malumbano na ujenzi wa makaburi hayo uendelee kwa ufadhili wake, na kazi hiyo imekuwa ikiendelea pamoja na kusafisha makaburi.

Taarifa iliyotolewa na mbunge huyo imeeleza kwamba, mafundi wanaojenga uzio huo wanahakikisha makaburi yaliyopo nje kidogo ya eneo la mpaka wa makaburi yanaingizwa ndani ya uzio ili kuyatunza yaendelee kuwa salama.

Chapisha Maoni

0 Maoni