Mwanafunzi ajinyonga na kuacha ujumbe mzito kwa wazazi

 

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lumbira iliyopo Kata ya Luanda Wilaya ya Mbozi mkoani hapa, Jafari Mwashitete (16) amekutwa amefariki shuleni akidaiwa kujinyoga.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya amedai kuwa walipokea taarifa ya kujinyonga kwa mwanafunzi huyo jana Jumatatu Julai 3, 2023 saa 10 jioni na kwamba ilikutwa karatasi mfukoni kwa mtoto huyo yenye ujumbe unaoeleza kutokutaka kusoma shule ya Lumbira badala yake anataka kusoma katika shule ya Myovizi.


ACP Mallya amesema Ujumbe huo unaeleza kwamba marehemu alitaka kusoma Myovizi lakini wazazi wake walimhamisha na kumpeleka Shule ya Sekondari Lumbila jambo ambalo hakulitaka.


Marehemu  Jafari alikuwa akisoma kidato cha tatu ambapo alihamia shuleni hapo akitokea Shule ya Sekondari Myovizi na kwamba mpaka umauti unamkuta alikuwa eneo la shule akiwa amevaa sare za shule.

Chapisha Maoni

0 Maoni