Rais Samia ashuhudia mkataba wa mabilioni kupiga jeki bajeti ya Tanzania


 Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza Tanzania kuendeleza ushirikiano na nchi za Ulaya uliodumu kwa zaidi ya miaka 48 sasa. Amesema msaada huo wa fedha utakwenda kusaidia maeneo muhimu ya utekelezaji wa bejeti.


Rais Samia ameyasema hayo baada ya hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya. 


Utiaji saini wa mikataba hiyo iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma,ambapo amesema Kiwango cha biashara baina ya EU na Tanzania kimeongezeka kutoka Dola za Marekani 1.3 bilioni mwaka 2019 hadi Dola 2.1 bilioni mwaka 2022.


Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema mikataba hiyo itakwenda kusaidia kuinua zaidi uchumi wa Tanzania kwa kuzigusa sekta mbalimbali kwenye utekelezaji wa bajeti.

Amesema fedha hizo zitakwenda kusaidia bajeti na maboresho ya sekta, jinsia, kidijitali, miji ya kisasa, uchumi wa buluu na kuboresha barabara za vijijini.

Naye Balozi Fantl amesema ana matumaini maeneo ya utekelezaji wa mikataba hiyo yatakwenda kuleta chachu katika fursa na ubunifu.

Chapisha Maoni

0 Maoni