Mpiga kinubi Siobhan aweka rekodi ya kupiga kinubi Mlima Kilimanjaro

 

Baada ya safari ya mchana na usiku kupanda Mlima Kilimanjaro mwanadada mpiga kinubi, kifaa chenye heshima kubwa nchini Ireland, Siobhan Brady, hatimae leo Julai 25, 2023, ameweka rekodi ya Dunia ya Guinness juu ya Mlima Kilimanjaro, Tanzania.

Siobhan ambaye mwaka 2018 aliweka rekodi Mlima Himalaya, India futi 16,000, leo ameitangaza Tanzania zaidi na Mlima wa Kilimanjaro kwa kuweka rekodi iitwayo “Guiness World Record for the Highest Harpist Concert” kwenye kilele cha juu zaidi duniani futi 19,000 Uhuru Peak.

Muda mfupi tu uliopita, Siobhan amefanikiwa kupiga kinubi kwa dakika 34, wakati ili kuvunja rekodi alitakiwa kupiga walau dakika zisizopungua 18 akichanganya nyimbo mbalimbali kutoka Ireland na mataifa mengine ya Ulaya.

Tukio hilo limerekodiwa na chombo kikubwa cha habari duniani The National Geographic. Sasa Kamati ya Dunia ya Guinness itakaa kuthibitisha rekodi hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni