Man United kumtwaa Hojlund kwa paundi milioni 72

 

Manchester United, imekubali mpango kuinasa saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark Rasmus Hojlund kutoka Atalanta ya ligi ya Sirrie A.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, atahamia Old Traford kwa dau la paundi milioni 64, pamoja na uwezekano wa kuongezewa tena paundi milioni 8.

Hojlund alijiunga na Atalanta Agosti 2022 na kufunga magoli 10 katika michezo 34 katika msimu uliomalizika.

Mkataba wake akiwa na United utakuwa wa miaka mitano, ukiwa na uchaguzi wa kuongezewa utakapomalizika.

Chapisha Maoni

0 Maoni