Bondia Crawford amdunda Spence na kuweka rekodi

 

Bondia Terence Crawford amemdunda Errol Spence Jr na kuwa mshindi wa kwanza wa mikanda minne asiyepingika katika ubingwa wa welterweight.

Bingwa huyo wa WBO mwenye umri wa miaka, 35, alimtwanga ngumi zilizomuangusha chini Spence mara tatu kabla ya refa kuamua kuingilia kati na kumaliza pambano raundi ya tisa.

Kwa ushindi huo umemfanya Crawford kuwa binadamu wa kwanza asiyepingika kwa kutwaa ubingwa wa mikanda ya mizani miwili tofauti.

Chapisha Maoni

0 Maoni