Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa amewasili nchini Urusi kuhudhuria mkutano wa pili wa kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi.

Mhe. Majliwa walipokelewa jana na kuongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Fredrick Kibuta kwenye uwanja wa ndege wa Pulkovo, St. Petersburg, Urusi.

Mhe. Majaliwa atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa pili wa kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa ya Afrika na Urusi.