Kibegi cha Simba kimebeba jezi zenye majina ya viongozi wa juu wa Serikali

 

Mtendaji Mkuu wa timu ya Simba SC Imani Kajula amesema kwamba jezi tano za timu hiyo zitakazo zinduliwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro zitakuwa na majina ya viongozi wa juu watano Serikali mgongoni.

Kajula ameyasema hayo na kutaja majina ya viongozi hao kuwa ni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ally Mwinyi.

Viongozi wengine ambao majina yao yamo kwenye jezi hizo ni Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson na Rais wa Heshima Mohamed Dewji Mo.

Chapisha Maoni

0 Maoni