Wahadhiri wapenda 'madenti' Nigeria kufungwa jela miaka 14

 

Bunge linalomaliza muda wake nchini Nigeria, limepitisha muswada unaolenga kuzuia ukatili wa kingono kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo.

Muswada huo utakapopitishwa kuwa sheria na rais mpya aliyechaguliwa, Bola Tinubu, itakuwa ni kinyume cha sheria kwa wahadhiri kuwataka kimapenzi wanafunzi wao.

Wahadhiri watakaobainika kuwa na mahusiano ya mapenzi na wanafunzi wao, watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Kumekuwapo na matukio ya wahadhiri kuwaomba ngono wanafunzi wao nchini Nigeria ili kuweza kuwapatia alama nzuri za ufaulu.

Chapisha Maoni

0 Maoni