Rubi kubwa ya Msumbiji yauzwa Dola milioni 35

Rubi kubwa kuwahi kupatikana imepigwa mnada na kuuzwa Jijini New York na kuweka rekodi ya kununuliwa kwa karibu dola milioni 35 za Marekani.

Jiwe hilo la madini lilikuwa na karati 55.22, lilibainika mwaka jana kwenye machimbo ya nchini Msumbiji.

Jiwe hilo la rubi, lilipewa jina la "Estrela de Fura” kwa lugha ya Kireno, ikiwa na maana ya "Nyota ya Faura".

Chapisha Maoni

0 Maoni