El Niño kusababisha joto kali duniani 2024

 

Hali ya hewa ya El Niño, imeanza kuwapo katika bahari ya Pacific, na huenda ikasababisha joto kali duniani, huku kukiwa tayari na joto linalosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wanasayansi wa Marekani wamethibitisha kwamba El Niño imeanza. Wataalam hao wameongeza kuwa kunauwezekano mwaka 2024 ukawa mwaka wa joto kali duniani. 

Hali hiyo itaathiri hali ya hewa duniani, kwa kuweza kuleta ukame nchini Australia, mvua zaidi kusini mwa Marekani na kudhoofisha upepo wa monsoon  India.

Chapisha Maoni

0 Maoni