Serikali yaandaa kanuni za wananchi kufanya biashara ya kaboni


Serikali imesema, imeandaa hatua na mikakati madhubuti yenye kuibua fursa za miradi ya kijamii kwa wananchi, ikiwemo kanuni na mwongozo wa biashara ya kaboni ikiwa ni njia mbadala ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Juni 2023 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi wakati akifunga warsha ya siku moja baina ya wahariri na menejimenti ya ofisi hiyo, iliyolenga kujenga uelewa kuhusu kanuni na mwongozo wa biashara ya kaboni.

Mitawi amesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na athatri za mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika hali inayojidhihirisha kupitia matukio ya mvua zisizotabirika, ongezeko la joto, ukame na mafuriko, ambapo athari hizo zimeathiri sekta za kijamii na kiuchumi.

“Pamoja na changamoto zinazochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwa na fursa na jitihada mbalimbali ambazo zimechukuliwa na serikali ikiwa ni pamoja na mapitio ya sera, uandaaji wa kanuni, mikakati na miongozo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mitawi.

Chanzo: editorsforums 



Chapisha Maoni

0 Maoni