Mwanamke aliyezinduka kwenye jeneza afariki tena

 

Mwanamke mmoja nchini Ecuador amefariki dunia siku chache tu kupita, tangu waombolezaji kubaini kuwa bado yupo hai akiwa kwenye jeneza.

Mwanamke huyo Bella Montoya, 76, alithibitishwa kuwa amefariki na daktari katika hospitali moja iliyopo kwenye mji wa Babahoyo wiki iliyopita.

Wakati wakiomboleza, waombolezaji walisikia jeneza linagongwa na walipofungua wakabaini bado yupo hai na kumkimbiza hospitali.

Baada kulazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi siku saba, Wizara ya Afya Ecuador ilithibitisha mwanamke huyo amefariki dunia siku ya Ijumaa.

Chapisha Maoni

0 Maoni