Rais Museveni asema amepona maambukizi ya corona

 

Rais Yoweri Museveni wa Uganda, amesema kwa sasa amepona maambukizi ya virusi vya corona, baada ya vipimo vya Covid-19 kuonyesha amepata maambukizi.

Kauli hiyo ya Rais Museveni ameitoa jana, ikiwa ni baada ya kupita siku 11 za kujitenga akipatiwa matibabu tangu kubaini kwamba anamaambukizi ya corona.

Rais Museveni amesema awali alidharau dalili za maambukizi, lakini alipoanza kupatwa na mafua ndipo alipomuita dokta ampime na kubaini amepata corona.

Haijajulina mara moja ni kwa jinsi gani Rais Museveni ambaye amekuwa akifuata taratibu kali za kujikinga na maambukizi ya Covid-19, amepata maambukizi hayo.

Chapisha Maoni

0 Maoni