Vita ya Ukraine lazima imalizike, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemuambia Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Kauli ya Ramaphosa
ameitoa alipokutana na Putin, St Petersburg siku ya Jumamosi akiwa ni sehemu ya
ujumbe wa wamani wa nchi sita za Afrika.
Ijumaa, Rais
Volodymyr Zelensky, aliuambia ujumbe huo ataingia katika mazungumzo ya amani
pale tu Urusi itapoondoka katika ardhi ya Ukraine.
Katika
maongezi yao na Putin aliwaambia viongozi hao wa Afrika kwamba Ukraine imekuwa
ikikataa kufanya mazungumzo ya amani.
Katika
mkutano wa St Petersburg, Ramaphosa alitoa wito kwa pande zote kurejesheana
wafungwa wa kivita na Urusi kuwarudisha watoto wanaodaiwa kuwachukua.
0 Maoni