Nyambizi yatoweka ikienda kuona mabaki ya Titanic

 

Nyambizi yenye watalii waliokuwa wanaenda kuangalia mabaki ya meli iliyozama ya Titanic katika pwani ya kaskazini ya Amerika imetoweka kwenye bahari ya Atlantic.

Vikozi vya ulinzi vya pwani ya Marekani vinakadiria kuwa nyambizi hiyo imebakiwa na saa 70 au 90, kabla ya mitungi ya dharura ya hewa ya oksijeni haijaisha.

Chombo hicho kina nahodha mmoja, na wataalam wanne wa msafara huo, kilianza kupigambizi siku ya Jumapili asubuhi.

Nyambizi ilipoteza mawasiliana baada ya muda wa saa moja na dakika 45, ilipopiga mbizi kwenda kuona mabaki ya Titanic, kwa mujibu ya Walinzi wa Pwani wa Marekani.

Mmoja ya watu wanaoaminika kwamba walikuwamo kwenye nyambuzi hiyo ni mfanyabiashara Muingereza na mvumbuzi Hamish Harding.

Mabaki ya meli ya Titanic yapo umbali wa mita 3,800m kwenye kina cha maji ya bahari, katika sakafu ya bahari.

Chapisha Maoni

0 Maoni