Mwanamke aswekwa jela kwa kuhamasisha ubakaji na utesaji

Mwanamke Mjerumani aliyejiunga na kundi la Dola ya Kiislam (IS), amefungwa miaka tisa jela kwa uhalifu ukiwamo wa kuwafanya watumwa wanawake wa kabila la Yazidi.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, pia alitiwa hatiani kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuwa mwanachama wa kundi la kigeni la kigaidi.

Mahakama ya mji wa magharibi wa Koblez, imesema mwanamke huyo aliwatesa wanawake wa Yazidi kwa miaka mitatu akiwa anaishi huko Syria na Iraq.

Pia Mahakama imebainisha kwamba mwanamke huyo alikuwa anamhamasisha mume wake kuwabaka na kuwapiga wanawake hao wa kabila la Yazidi.

Chapisha Maoni

0 Maoni