Arsenal yaelekea kumtwa Kai Haverts kutoka Chelsea

 

Timu ya Arsenal imekubali kulipa dau inalohitaji Chelsea la paundi milioni 65 ili kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz.

Imefahamika kuwa klabu hizo zimefikia makubaliano ya msingi, yanayotoa nafasi kwa mchezaji huyo kujadili maslahi yake na kufanyiwa vipimo vya afya.

Ada ya Havertz, ambaye amefunga magoli tisa katika michezo 47, akiwa na Chelsea msimu uliopita, itakuwa na nyongeza akipata mafanikio.

Havertz, 24, alijiunga na Chelsea akitokea timu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani mwaka 2020 kwa dau la paundi milioni 71.

Chapisha Maoni

0 Maoni